O
Ushirika mzuri ni ule ambao umejaa msamaha na toba. Iwe kativya sisi kwa sisi yaani binadamu pamoja na Mungu,
Neno la Bwana linasema msiyakumbuke mambo ya kwanza wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama nitatenda jambo jipya............... (Isaya43:18-19)
Kumbe kukumbuka na kutafakari mambo ya zamani kunaweza kuvuruga ushirika na kusimama kama kikwazo cha mambo mapya kutendeka.
Tazma pia Mathayo 6:14
2wakoritho 5:17
hata imekua mtu akiwa ndani ya kristo amekua kiumbe kipya yakale yamepita tazama yamekua mapya
Hapa biblia inaonesha jinsi mtu anavyokua na ushirika na Mungu anatakiwa kua
1.anakua kumbe kipya.
Upya huu unaoupata baada ya kua ndani ya kristo ndio unaoboresha ushirika wetu na Mungu.
Sehemu moja katika biblia inasema
( mtu hatii divai mpya katika kiriba kikuukuu ). Hivyo inatupa ujasiri kusema unapokua kumbe kipya tayari unaruhusu Mungu akutumie kwa kuwekeza ndani mwako.
Unapokua kumbe kipya unatoa nafasi ya kuimarisha ushirika wako na Mungu.
2.Ya kale yote yamepita .
Biblia inapozungumza mambo ya kale inazungumza juu ya tabia za asili za mwanadamu ambazo hazitendi mapenzi ya mungu.
Tabia za mambo ya kibina damu ambalo yametajwa katika Wagalatia 5:19-20 .
Tabia hizi ndio hutenga mbali na Mungu na kuharibu ushirika.
Petro alimuuliza yesu kua tumeacha vyote je tutapata nini basi tukikufuata wewe?
Kumbe ushirika wa petrol na Yesu ulikua nikuacha vyote na kumfuata Yesu.
Tukumbuke yakua Petro ulikua mvuvi alikubali kuacha vyote pamoja na kwamba alivipenda na alipenda kazi yake lakin bado alikubali kuiacha.
Kuna mambo ambayo awali yalikua mazuri kwako pengine yalikufaidisha lakini unapomgeukia Mungu na kwanza ushirika na Mungu unatakiwa kuyaacha.
* Vivyobhivyo hata kwa wanadamu wenzetu, ambapo ushirika wetu na wanadamu wenzetu ndio inaonesha jinsi gani tuko vizuri na Mungu. (Utasemaje wampenda Mungu wakati jirani yako unamchukia).
Chuki inatokana na kushindwa kusamehe kwa muda mrefu. Unaweza usiwe na chuki lakini ukawa na ushirika mbaya na wenzako ambapo unajikuta unapata matokeo hasi.
Unapokuana chuki juu ya mtu, ushirika kati yako na yeye unakua hafifu.
Watu wengi wamepata matatizo katika maish ikiwa chanzo ni ushirika mbaya.
Biblia inasema watu wawili wawezaje kutembe njia moja kama hawajapatana?
Na upatano unatokana na ushirikamzuri.
Pia mithali 1:10 biblia inasema "mwanangu mwenye dhambi akikushawishi wewe usikubali"
Hii inaonesha kua ushirika ukikomaa unaleta ukaribu kiasi cha kushauriana.
Comments
Post a Comment