Translate

Washindi na walioshindwa michezo ya Jumuiya na madola Gold Coast

Wenyeji wa mashindano hayo huko Gold Coast - Australia wanaongoza na dhahabu 39, Uganda ikiwa katika nafasi ya 12, Kenya ya 21 na Mauritius ya 23.

Timu ya Rwanda ya voliboli ya ufukweni jana imeshinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Singapore
Fathiya Pazi amemshinda mpinzani wake wa Tuvalu 4-0 na hivyo kuwa mchezaji pekee wa Afrika Mashariki kuibuka mshindi mechi za tenisi ya meza kufikia sasa

Akishinda mechi yake ya pili leo jioni ya tenisi ya mezani, Fathiya Pazi ataingia awamu ya mtoano.

Bondia wa Uganda Juma Miiro amemshinda Shafi Bakari wa Kenya uzani wa light-fly na kufuzu nusu-fainali hivyo basi kuihakikishia Uganda medali ulingoni

Shafi Bakari wa Kenya aliibusu sakafu raundi ya pili na kuhesabiwa hadi nane. Matumaini ya Kenya sasa yako kwa Christine Ongare uzani wa fly anayecheza kesho na bondia wa Sri Lanka

Masoud Mtalaso wa Tanzania (kushoto) na Halima Nambozo wa Uganda wote wamepoteza mechi zao za kwanza katika mchezo wa tenisi ya mezani.

Comments