Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa
Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, George Lwandamina amefunguka na
kudai walilazimika kubadili mbinu za mchezo kutokana na hali ya
mazingira kuwa tofauti na wao walivyozoea.
Lwandamina
ameeleza hayo asubuhi ya leo kupitia ukurasa wao maalum wa klabu baada
ya timu yake kutoka kifua mbele siku Jumapili kwa kuwachakaza
Njombe Mji FC kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Ibrahim Ajib kwa
kutumia mkwaju wa adhabu.
"Tulijua utakuwa mchezo
mgumu, kipindi cha pili tulilazimika kubadili mbinu ili kukabiliana na
mazingira. Nawashukuru wachezaji hakika walifanya kazi kubwa dakika zote
90 za mchezo", amesema Lwandamina.
Kwa upande mwingine, timu ya Mtibwa
Sugar kwa sasa ndiyo ambayo inaongoza ligi kwa mujibu wa msimamo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara kwa pointi sita, akifuatiwa na Simba SC kwa pointi
nne, Tanzania Prisons alama nne

Comments
Post a Comment