Mbunge Joseph Mbilinyi, ‘Sugu’ amedai
marufuku ya jeshi la Polisi kuzuia maombi maalum kwa ajili ya Tundu
Lissu haitaathiri afya yake kwani yeye anaamini viongozi na wanachama wa
chama waliotangulia mbele za haki wanamuombea moja kwa moja kwa Mungu
Sugu
aliyasema hayo wakati wa Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa viti
Maalum kupitia (CHADEMA) jiji la Mbeya Esther Mpwiniza aliyefariki dunia
ghafla Septemba 16, mwaka huu kutokana na Shinikizo la damu.
Sugu alisema kwa kuwa jeshi la polisi limezuia ibada kwa ajili ya
kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa
CHADEMA Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana yeye anaamini wanachama waliotangulia mbele za haki
watafanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama.
Sugu aliendelea kusisitiza kuwa mbali na kupiga marufuku kufanya
maombi pia serikali imekuwa ikiwazuia watu kwenda kwenye misiba ambapo
alidai viongozi na wanachama walizuiwa kuhudhuria msiba wa aliyekuwa
mbunge wa Moshi Mjini Marehemu, Philemon Ndesamburo.
“Naamini Kamanda wetu Esther
saizi upo moja kwa moja na Malaika naomba ukamuombee Tundu Lissu apone
haraka anyanyuke kutoka kitandani aendelee na kazi za ukombozi wa taifa
letu, huku wametuzuia kufanya maombi lakini huko najua hawezi kufika
kuwazuia,”alisema Sugu
Akizumzungumzia marehemu Mpwiniza Sugu alisema alikuwa ni mwalimu wa
siasa na mpiganaji wa kweli kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa jiji la
Mbeya pamoja na chama na kwamba mchango wake umefanikisha ushindi wake
kwa kiwango kikubwa. Amedai marehemu alikuwa ni ngao na mtu mwenye tabia
ya kuwaunganisha wanachama na kuondoa tofauti ambazo zililkua zinatoa
mwanya wa kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho
Comments
Post a Comment