Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametolea ufafanuzi suala la matibabu ya
mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu
Antiphas Lissu aliyepelekwa Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa
risasi.
Akitoa
taarifa hiyo mara baada ya sala ya kuliombea bunge asubuhi ya leo ili
kuanza vikao, Spika Ndugai amesema utaratibu wa matibabu kwa mbunge
yeyote ulikuwa umeshafuatwa lakini familia iliamua yenyewe kumpeleka
Nairobi, na siyo kama walishindwa kumpeleka nchini India.
"Baada ya bunge kupata taarifa kuhusu tatizo hilo, sisi bunge
tulikuwa tumeshaagiza ndege tayari ilikuwa uwanjani, hapa Dodoma kwa
ajili ya kumpeleka Hospitali ya Muhimbili ambapo ndiyo utaratibu wa
kibunge, na kama kuna rufaa ya nje ya nchi utaratibu wetu ni kwamba
serikali yetu ina mkataba na hospitali ya Apolo kule India, na ndiyo
'channel' ya sisi wote. Lakini kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni
kwa sababu familia iliomba na Mh. Mbowe alieleza na mimi nilinukuu kwa
niaba yake, walisema siyo kama wana mashaka na umahiri wa madaktari
wetu, lakini wangejisikia faraja kwa wao wenyewe kuachagua kumpeleka
kutibiwa Nairobi", alisema Spika Ndugai.
Spika Ndugai aliendelea kusema kwamba tukio la kupigwa risasi kwa
Tundu Lissu ni la kwanza tangu historia ya bunge kuhamia Dodoma kwa
miaka mingi, na kulivitaka vyombo vya dola kushughulikia tatizo hilo,
huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu kwani hali yake inatia moyo
Comments
Post a Comment