Mtuhumiwa wa utekaji wa watoto Arusha,
Samson Peter amefariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu
kuwakimbia Polisi alipokuwa amekwenda kuwaonyesha washirika wenzake wa
utekaji eneo la Muriet Mkoni Arusha.
Mtuhumiwa wa Utekaji, Samson Peter
Akithibitisha
kutokea kwa kifo chake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
amesema kuwa mtuhumiwa huyo wa utekaji alipigwa risasi ya mguuni kama
onyo la kujaribu kumtoroka Askari aliyekuwa ameongozana naye majira hayo
ya saa 5:30 usiku.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa baada ya
tukio hilo la kumjeruhi mtuhumiwa Samson Peter kwa nia ya kumuadhibu
alifikishwa Hospital ya Mt. Meru lakini alifariki kutokana na kuvuja
damu nyingi kwenye jeraha la mguu.
"Ni kweli mtuhumiwa
amefariki. Ambapo jana usiku wakati alipokuwa amesindikizwa na polisi
kuwaonyesha waashirika wenzake alitaka kutoroka, lakini katika hatua ya
kumuadhibu kwa kitendo chake hicho ndipo akapigwa risasi ya mguuni
ambapo ilimpelekea kuvuja damu nyingi na alifariki baada ya kufikishwa
hospitali" amesema Kamanda Mkumbo akizungumza na mwandishi wa EATV.
Comments
Post a Comment