Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma,
ametoa taadhari kwa Majaji wafawidhi kuwa makini na matumizi ya mitandao
ya kijamii katika mahusiano pamoja na kutoa michango kwenye mitandao
hiyo juu ya jumbe zisizofaa.
Jaji Mkuu ametoa angalizo hilo wakati akifunga mkutano wa Majaji wafawidhi wa kanda nchini, uliofanyika Jijini Arusha
"Katika suala la matumizi ya
mitandao, kuweni makini. Msi- like picha ambazo hazina maadili au
kuchangia kwa kutoa maoni katika mitandao ya kijamii," alisema.
Aidha, amewataka kuwa makini na ndugu au jamaa wanaowatembelea, akisema baadhi yao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali ya kijinai.
Aliwataka majaji hao kujenga tabia ya
kupenda kujisomea na kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge kwa
kurekebisha sheria ili kuweza kugundua makosa mbalimbali yanayofanywa na
Mahakama za chini na wafundishane namna ya kuboresha hukumu
zinazotolewa ili kupunguza mrundikano wa mashauri.
"Ni vizuri kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge wakati wa kurekebisha sheria, kazi na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kufungua mashauri," alisema.
Kuhusu migongano kati yao na vyombo
vingine vya serikali, aliwataka kutambua mipaka ya vyombo hivyo na wao
watambue mipaka yao huku akisisitiza kwamba kila chombo kikitambua
mipaka yake wataheshimiana na hakutakuwa na mgongano katika utekelezaji
wa majukumu yao.
Comments
Post a Comment