Mahakama imemuachia huru Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu katika
kesi iliyokuwa inawakabiri ya kushindwa kuhifadhi silaha baada ya upande
wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo.
Gwajima
na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo leo Jijini Dar es Salaam,
mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe na kuamuru
arudishiwe mkoba wake wenye silaha.
Katika kesi hiyo ambayo Gwajima alikuwa
akisimamiwa na Wakili Peter Kibatala walishtakiwa hao ambao msaidizi
wake Gwajima, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43)
na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31) mnamo Machi 29 mwaka
2015 walikutwa katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A,
wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na
kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Comments
Post a Comment