Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Jeshi la Wananchi
kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta mkubwa kuzunguka eneo lenye
madini ya Tanzanite na kuweka mitambo maalum, ili kulinda madini hayo
yasiendelee kuibiwa.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambako
ameende kuzindua barabara ya lami iliyojengwa kwa bilioni 32.5 ya KIA-
Manyara, na kusema kwamba ni lazima ulinzi huo uwekwe ili kuokoa
rasilimali za Tanzania zisiendelee kuibiwa na nchi kubaki masikini.
"Eneo la Simanjiro kuanzia Block A mpaka Bolock D ambalo lina madini mengi, ninaagiza Jeshi la wananchi likishirikiana na Suma JKT, waanze kulijengea ukuta eneo lote, wataweka fensi juu na wataweka camera, patawekwa mlango mmoja na itawekwa mitambo maalum, hata kama utameza Tanzanite itaonekana, hata ukificha kwenye kiatu itaonekana", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli atakuwepo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3, ambapo pia atatoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Septemba 23, 2017.http://www.eatv.tv/news

Comments
Post a Comment