Korea Kusini inasema kuwa
kuna dalili kuwa Korea Kaskazini inapanga majaribio zaidi ya makombora
hususan makombora ya masafa marefu.
Maafisa wa ulinzi wamekuwa wakilishauri bunge mjini Seoul baada ya Korea kulifanyia jaribio bomu la nyuklia mwioshoni mwa wiki.
Korea Kusini imejibu kwa kufanya majaribio kwa kurusha makombora kwa kutumia ndege na kutoka ardhini.
![]() | |
| Korea Kusini ikifanya majaribio la kombola leo Jumatatu |
Marekani imeonya kuwa tisho lolote kwake na kwa washirika wake litapigwa vikali kijeshi.
Korea Kusini inasema kuwa ililifanyia majaribio bomu la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.
Chang
Kyung-soo, ambaye ni afisi kutoka wizara ya ulinzia aliliambia bunge,
"tunaendelea kuona dalili za uwezekano wa makombora zaidi ya masafa
marefu. Pia tunaweza kutabiri kuwa Korea Kaskazini huenda ikarusha
kombora la masafa marefu.
Wizara hiyo pia ililiambia bunge kuwa huenda Marekani ikapeleka manowari wa nyuklia ya kubeba ndege katika rasi ya Korea
Korea Kusini imefanya mazoezi ya makombora yake kuashiria shambulizi
dhidi ya Korea Kaskazini, kujibu jaribio la sita la nyuklia lililofanywa
na Korea Kaskazini.

Comments
Post a Comment