Syria inasema kuwa
ndege za jeshi la Israeli zimeshambulia kituo cha kijeshi magharibi mwa
nchi huku ripoti zikiseka kuwa kiwanda cha silaha za kemikali
zilishambuliwa.
Taarifa za jeshi zilisema kuwa makombora
yaliyofyatuliwa kutoka anga ya Lebanon yalilenga kiwanda hicho kilicho
karibu na Masyaf na kuwaua wanajeshi wawili.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kiwanda ya kutengeneza silaha za kemikali kilishambuliwa
Israeli ambayo imefanya mashambulizi kadha kwenye viwanda vya silaha nchini Syria awalia haijasema lolote.
Kisa
hicho kinatokea siku moja baada wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kusema
kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulizi la silaha za kemikali
katika mji unaoshilkiliwa na waasi mwezi Aprili.
Takriban watu 83 waliuawa katika mji wa Khan Sheikhoun na Styria imekana kutumia silaha za kemikali.
Ujasusi wa nchi za magharibi unasema kuwa Syria inandelea kuunda silaha za kemikali.
Isarel inaripotiwa kuendesha mashambulizi ya ndega maeneo yanayotajwa kutumika kuunda silaha za kemikali miaka ya hivi karibuni.
Hivi karibuni Isreal iliishitumu Syria kwa kuruhusu hasimu wake
Iran kujenga viwanda vya makombora nchini humo na inasema inalenga
kuzuia kupelekwa kwa silaha kutoka Syria hadi kwa wanamgambo wa Lebanon,
Hezbolllah.

Comments
Post a Comment