kimbunga kingine kikubwa kulikumba eneo la Caribbean
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Eneo la Caribbean lajiandaa kwa kimbunga kingine kikubwa
Kimbunga Maria kinatarajiwa kuwa kibunga hatari wakati kinakaribia visiwa vya Leeward eneo la Caribbean.
Kimbunga
hicho cha kiwango cha kwanza kitapata nguvu kwa haraka ndani ya saa 48
zinazokuja na kugonga visiwa hivyo baadaye leo Jumatatu, huku kikitarajiwa kunapitia eneo ambalo kimbunga Irma kilipitia. Onyo la kimbunga limetolewa maeneo ya Guadeloupe, Dominica, St Kitts na Nevis, Montserrat na Martinique.
Tahadhari
ya kimbunga kwa sasa inachukuliwa nchini Marekani na visiwa vya
Uingereza vya Virgin, St Martin, St Barts, Saba, St Eustatius na
Anguilla. Baadhi ya visiwa hivyo bado vinajaribu kurejea hali
ya kawadia baada ya kupigwa na kimbunga cha kiwango cha tano,
kilichosababisha vifo vya takriban watu 37 na hasara ya mabilioni ya
dola. Kwa mujibu wa utabiri wa kwanza kimbunga Maria
kitapitia visiwa vya Leeward baadaye Jumatatu na Jumatatu usiku kisha
kielekee maeneo ya kusini mashariki mwa bahari ya Caribbean siku ya
Jumanne na Jumanne usiku
Comments
Post a Comment