Kimbunga Irma kimepiga jimbo la
Florida nchini Marekamani, ambapo awali kilikikumba kisiwa cha Marco magharibi mwa pwani mwa
Florida, kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 192 kwa saa lakini kwa sasa
kimeshuka kutoka kiwango cha tatu hadi cha pili.
![]() |
| Gari ikiwa imeangushwa na mafuriko katika mtaa wa Miami |
Zaidi ya nyumba milioni 3.4 katika
jimbo la Florida zimekosa nishati ya za
umeme huku sehemu za mji wa Miami zikifurika maji.
Vifo vitatu vinavyotokana na kimbunga
hicho vimeripotiwa wakati kimbunga hicho kikielekea sehemu za Kaskazini
Kituo kinacho husika na vimbunga
nnchini Marekani kinasema kimbunga hicho
kimesababisha upepo sehemu tofauti za katikati mwa Florida.
Mapema kimbunga hicho kilipiga
maeneo yanayozunguka mji wa Fort Myers, huku kikiharibu maeneo ya Caribbean na
kuuwa takribani watu 28.
Kutokana na hali hiyo takribani watu milioni 6.3 huko Florida
wameambiwa wahame.

Comments
Post a Comment