atoa neno kuhusu wasiojulikana
Watetezi wa haki za binadamu kwa umoja
wao wametaka watu wasiojulikana waweze kuchukuliwa hatua za kiusalama
mara moja ili kubaini wahalifu hao wanajihusisha na vitendo vya kikatili
dhidi ya watu mbalimbali nakuzuia hali hiyo isiendelee kutokea tena.
Dkt Helen Kijo-Bisimba
Akizungumza
leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za binadamu, Dkt
Helen Kijo-Bisimba amesema kwamba matukio hayo kukomeshwa kutajenga
amani na umoja kwa watu.
Kama hatua za kisheria na za kiusalama
hazitachukuliwa kwa tukio hili la kinyama litaleta shida kwa taswira ya
nchi ya Tanzania kwenye nchi zingine na kuchafua serikali. Kwani hakuna
nchi duniani iliyoingia katika kadhia hizi ni zikabaki salama" Bi
Kijo-Bisimba
Pamoja na hayo watetezi hao wamemuunga mkono Rais kutokubali kunyonga baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kifo
Mbali na hayo Kituo hicho kimewataka
viongozi wa dini kuchukua hatua madhubuti kukemea kwa nguvu kubwa
matukio hayo kwani mwisho wa matukio haya ni kuvunjika kwa amani ya
nchi.Pia amewataka viongozi wa siasa kujadili masuala ya usalama na haswa suala la utekwaji na mashambulizi ya kinyama kwa wananchi na kutoa mapendekezo yatakayoleta suluhu ya kudumu kwa usalama wa nchi
Comments
Post a Comment