"Katika serikali yeyote ambayo inawajibika ipasavyo kazi ya kwanza ya serikiali ni kulinda uhai wa wananchi wake"-Sumaye
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Fredrick Sumaye amedai endapo
serikali ingekuwa inawajibika ipasavyo, matukio ya kiuhalifu yasingekuwa
yanaendelea kujitokeza mara kwa mara nchini.
Mhe.
Sumaye ameeleza kupitia mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam leo ikiwa imepita siku moja tokea kwa tukio
lililompata Mhe. Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake
mjini Dodoma 'Area D' na watu wasiofahamika.
Aidha Sumaye ameeleza kuwa "kwa
sababu serikali ni yetu sote bila ya kujali itikadi ya chama husika.
Kwa hiyo mimi nasema kama kweli serikali inawajibika inavyotakiwa basi
haya mambo yote ambayo yanatokea yalitakiwa yapatikane majibu ya uhakika
na kwani yanapoachwa baadhi ya maeneo yapo gizani basi wengi tunaanza
kufikili kwamba utawala unaowajibika unakosekana ama kwa makusudi au kwa
uwezo".
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti
wa chama hicho Prof. Abdallah Safari amesema kabla ya Mhe. Tundu Lissu
kupigwa risasi alikuwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa juu ya maisha yake
kutokana na baadhi ya watu waliokuwa wanamfuatilia kwa ukaribu kila
kukicha.
"Kabla ya tukio hili kutokea
Mhe. Lissu alishawahi kusema katika mkutano wake na waandishi wa habari
alikuwa na hofu na maisha yake kutokana na kufuatiliwa na watu wenye
gari aina ya Nissan Premier yenye namba za usajili T460 CQV hapa hapa
Dar es Salaam. Kwa hiyo maisha ya Lissu yamekuwa yapo hatari kwa kipindi
kirefu", amesema Prof. Safari.
Kwa upande mwingine, Prof. Safari
amevitaka vyombo vya usalama vitekeleze kazi zake kwa uweledi kama
ambavyo wanaweza kufanya katika matukio mengine ya kiuhalifu.

Comments
Post a Comment