Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema anaamini ipo siku
nyota wa zamani wa timu hiyo Wayne Rooney atarejea klabuni hapo.
Mourinho
amesema hayo mbele ya waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu mapokezi
ya Rooney kwenye mchezo wa jana kati ya Manchester United dhidi ya
Everton ambapo mashabiki walimpokea nyota huyo kwa shangwe nyingi.
"Rooney hana tatizo na timu wala mimi
sina tatizo na Rooney ndio mana tumesalimiana kwa furaha, naamini siku
moja atarejea maana hapa ni nyumbani kwake hata mashabiki wamempokea
vizuri" amesema Mourinho.
Rooney jana alirejea kwa mara ya kwanza
kwenye uwanja wa Old Trafold tangu aondoke kwenye dirisha la usajili
lililopita ambapo alirudi kwenye timu yake iliyomkuza ya Everton na jana
ilikumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa United.
Rooney ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Manchester United akiwa na mabao 253.

Comments
Post a Comment