Translate

Jaji mkuu mpya atoa neno baada ya kuapishwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alimteua kushika wadhifa huo Septemba 10, mwaka huu.
Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma akiwa Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, ikihudhuriwa  na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Majaji wengine wa Tanzania.

Jaji Ibrahim Juma aliyeapishwa amesema anashukuru kwa kurasimishwa kushika wadhifa huo, ambao alikuwa ana ukaimu takriban miezi nane mpaka alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Katika hotuba yake ya kwanza Jaji Mkuu Ibrahim Juma ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi ikiwemo kulinda sheria na kuweka imani kwa wananchi, kwani wao ndiyo watetezi wao.

"Jambo ambalo ni muhimu kwetu sisi katika kufanya kazi ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na imani ya wananchi, kwa sababu wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama hawatakuja kwetu ili kutatua matatizo yao. Sisi tumejiwekea mipango ya kuhakikisha tunaendelea kupata imani ya wananchi wetu, na tutafanya hivyo kwa kuepuka utovu wa maadili, vitendo vya rushwa na ucheleweshaji wa mashauri", amesema Jaji Mkuu Ibrahim Juma.
Ibrahim Juma alianza kutumikia wadhifa wa Kaimu Jaji Mkuu tangu Januari 18 mwaka 2017, chini ya  aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kustaafu.

Comments