Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Simon Sirro amefunguka na kusema watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga
risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa wanaweza patikana
ikiwa wananchi watasaidia jeshi hilo kupata taarifa za wahalifu hao.
"Naomba wananchi
wasidanganywe kwenye suala zima la siasa na vitu vingine hapa huwa
nasema siku zote kama hakuna amani na usalama siasa haiwezi kupata
nafasi ili tukio limetokea tunapeleleza na tupo makini na hili tukio,
kwa sasa tumeongeza vikosi vya upelelezi Dodoma, wale waliofanya lile
tukio ni lazima tutawakamata ila upelelezi huu unaweza kuzaa matunda
mazuri zaidi endapo wananchi watatupa ushirikiano wa kutosha" alisema IGP Sirro
Comments
Post a Comment