Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman
Mbowe amesema ile hofu iliyokuwepo ya Mbunge Tundu Lissu
aliyeshambuliwa na risasi kuwa huenda angepoteza maisha imezidi kupungua
na kueleza kwamba madaktari wanatoa matumaini makubwa hali yake inaimarika.
"Kuhusu hali ya Mhe. Lissu,
kwa sasa ile hofu ya kupoteza maisha imezidi kupungua, madaktari sasa
wanatoa matumaini makubwa kuwa hali yake sasa inaimarika. Yale yote
yaliyokuwa yanatishia pengine uhai wake, usalama wake, yamepungua kwa
kiasi kikubwa na madaktari wanatoa matumaini makubwa. sasa hivi, Mhe
Lissu anaweza kuzungumza, nimezungumza nae, japo bado anapatiwa matibabu
na ataendelea kwenda 'theatre' kwa ajili ya upasuaji na kutibu majeraha
mbalimbali aliyoyapata. Anazungumza na anatoa salamu kwa Wanaafrika
Mashariki, anatoa salamu kwa Watanzania, niseme tu kwamba sisi ambao
tuko nae muda wote ndo tunajua hali halisi ya mgonjwa" alisema Freeman Mbowe
"Mhe. Lissu hana 'infection'
ya kifua, kwa sasa yuko vizuri yuko imara, bado ni 'critical' lakini
bado yuko stable. Tuendelee kumuombea kila siku, wakati wote, aweze
kupona kwa haraka na kuruhusiwa kutoka hospitali" alisema Mbowe
Comments
Post a Comment