![]() |
| Refa raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimamia mechi kwa njia isiyofaa |
Mechi ya kufuzu
kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal itarudiwa tena baada ya
refa aliyesimamiwa mechi hiyo kupigwa marufuku na Fifa.
Refa huyo raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimia mechi kwa njia isiyofaa.
Aliwapa
penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1 mwezi Novemba
mwaka uliopita kwa kunawa mpira lakini kanda ya video baaadaye ilionyeha
kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal Kalidou
Koulibaly.
Mechi hiyo itachezwa tena Novemba mwaka huu.
Lamptey alipigwa marufuku mwezi Machi lakini jana Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo.
![]() |
| Fifa yalazimisha mechi kati ya Afrika Kusini na Senegal kuchezwa tena |
Senegal na Afrika Kusini kwa sasa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi la la D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.
Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa mechi za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.


Comments
Post a Comment