Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa
taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida
Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa
leo.
Shambulio
hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na
kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.
CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.
CHADEMA MAKAO MAKUU
DAR ES SALAAM

Comments
Post a Comment