Kesi inayowakabili viongozi wa juu wa
klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa hadi
Septemba 27 mwaka huu, huku upelelezi wao ukiwa umekamilika na jalada
lao kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Hayo
yamebainishwa leo na Wakili wa serikali, Nassoro Katuga na kumueleza
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria
Nongwa kuwa upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika na jalada
limepelekwa kwa DPP ili aweze kulipitia na kuona kama umekamilika au laa
Mara baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa ameamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo na kusikilizwa tena hadi Septemba 27 mwaka huu.
Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi michache iliyopita
wakikabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya
kutakatisha fedha
Comments
Post a Comment