Translate

Tamasha la michezo la wanawake kufanyika kesho

MAKAMU Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la michezo la wanawake linalotarajiwa kufanyika kesho uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Baraza la Michezo la taifa(BMT) kwa ajili ya 
kuwakutanisha wamama kutoka maeneo mbalimbali nchini linatarajiwa kuanza saa 12 mpaka saa 5 ya asubuhi.

Ofisa habari wa BMT, Najaha Bakari alisema tamasha hilo linatarajiwa kuwa na mvuto wa kipeke yake kutokana na kujumuisha michezo mbalimbali kwa wamama ambayo itaonesha na kuleta muunganiko na ushirikiano baina yao.

Alisema licha ya kuwepo kwa michezo mbalimbali siku hiyo pia kutakuwa na fursa ya kupata burudani kutoka vikundi mbalimbali vya shule za msingi na sekondari 
vilivyoandaliwa na wataalamu wenye uwelewa mkubwa wa masuala hayo.

"Katika tamasha hili hakuta kuwa na kiingilio cha aina yoyote ile kwa hiyo niwaombe 
wamama wenzangu wajitokeze kwa wingi kuja kwenye hili tamasha kwa sababu wataondoka na mambo mengi yatakayowasaidia katika maisha yao," alisema Najaha.

Pia Najaha alitoa shukrani kwa wadau mbalimbali waliojitokeza na kuwachangia 
gharama mbalimbali ambazo zimefanikisha kuwepo kwa tamasha hilo kwani kulikuwa na vitu lukuki walivyokuwa wanaupungufu navyo vikiwemo maji pamoja na Tisheti kwa watakaoshindana kwenye riadha.

Hata hivyo Najaha aliongeza kuwa Siku hiyo pia kutakuwa na tukio maalum la upimaji afya bure ambalo litafanywa kwa wamama wote pasipo kuangalia tofauti zao za kifedha kwani wanaamini kufanya hivyo wataokoa maisha ya wamama wengi wa kitanzania ambao wengi wao wanaishi katika hali ya kipato cha chini.

Comments