HATIMAYE Uongozi wa Klabu ya Simba umekamilisha taratibu za kuzikomboa Nyasi bandia za timu hiyo zilizokuwa zikishikiliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kosa la kutolipia ushuru wa forodha kwa wakati.
Makamu wa Rais wa Simba, Gofrey Nyange'Kaburu' alisema nyasi zao ziliwasili nchini muda mrefu lakini hawakufanikiwa kwenda kuzichukua kwa wakati kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha.
Alisema kwa sasa wakala wao ambaye anayeshughulikia suala la nyasi hizo yupo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha jukumu la kuchukua baadhi ya nyaraka ili wazitoe nyasi hizo na kwenda kuendelea na mipango yao waliyojiwekea.
Kaburu alisema mara baada ya nyasi hizo kutoka wanatarajia kuendelea na program ya utengenezaji wa uwanja wao wa Bunju ili kuhakikisha wachezaji wao wanafanyia
mazoezi katika uwanja huo pindi msimu mpya wa ligi wa 2017/18 utakapokuwa umeanza.
Tunafurahi jambo hili limekwenda vizuri na kiukweli tulikuwa tukiumiza sana vichwa
vyetu juu ya kulipatia ufumbuzi sakata hili kwa sababu lilikuwa likiturudisha nyuma
kimaendeleo maana Sisi kama Simba tulishajiwekea malengo yetu na kwa upande fulani hayajaenda kama vile tulivyotaka," alisema Kaburu.
Hata hivyo Kaburu aliendelea kuwashukuru wanasimba kwa kuwa wapole kwa muda wa siku chache zilizopita tangu waliposikia taarifa za uzishi kutoka katika mitandao ya kijamii juu ya uuzwaji wa nyasi bandia za timu hiyo ambapo kama waanzishe vurugu basi wangejikuta inawawia vigumu kumalizana na TRA kwa muda wa siku chache zilizosalia.
Wakati huo huo, Kaburu alisema wachezaji wa timu yao bado wanamorali kubwa ya
kuendelea kupambana na wapinzani wao Mbao Fc katika mchezo wao utakaofanyika Jumatatu katika uwanja wa CCM Kirumba licha ya kupata matokeo mabaya katika mchezo wa ligi kuu ulioffanyika wiki iliyopita.
Alisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog amekaa na wachezaji wake katika program yao ya mazoezi yaliyofanywa kwa siku tatu mfululizo na wameelezwa mapungufu waliyokuwa wameyaonesha katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ulimalizika kwa kupewa kichapo cha mabao 2-1.
Pia alisema timu hiyo inatarajia kuanza safari yake mchana wa leo mara baada ya
kuweka kambi ya Siku tatu mkoani Geita na wanatarajia Kocha atakuwa akiendelea na program ya mazoezi kama alivyopanga mpaka siku ya jumatatu ambapo mchezo wao utafanyika.
"Niwaombe wanasimba wasivunjike moyo bado tunaendelea vyema na tunatarajia
tutafanya vyema katika mchezo wetu dhidi ya Mbao Fc tutakaoucheza jumatatu kwa
sababu ili tuchukue ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara basi hatuna budi kuonesha
kile tulichonacho," alisema Kaburu.
Comments
Post a Comment