Translate

TFF yakanusha taarifa ya msamaha kutoka Young Africans








SHIRIKISHO la mpira wa Miguu nchini(TFF) limekanusha kupokea barua ya kuomba msamaha kutoka kwa mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Young Africans,Jerry Murro ambaye anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Afisa habari wa wa TFF, Alfred Lucas alisema pamoja na kusambaa kwa taarifa zinazodai kuwa Jerry Muro aliandika barua ya kutaka apunguziwe adhabu kama si kusamehewa, bado hawajapata uthibitisho huo kwa maandishi.
"Mimi mwenye nimemsikia Muro akisema amekwenda moja kwa moja kwa Rais kupeleka barua yake ya kuomba msamaha, na pia nataka niwaambie watanzania kwamba kama Muro angeleta barua yake kwa yeyote kwenye ofisi za TFF basi tungekuwa na taarifa hizo kwa sababu sisi ndio watendaji na wakati wote tupo hapa ofisini," alisema Lucas.
Alisema wao wenyewe wamesikia Muro akizungumza kwenye vyombo vya habari juu ya kuomba msamaha kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ili ampatie msamaha kwa makosa aliyobainika kuyafanya kabla ya kushushiwa rungu la adhabu hapo mwaka jana.

Inadaiwa Muro alifikishwa katika kamati ya maadili kwa makosa makubwa matatu na baadae kubainika kutenda makosa mawili huku kubwa zaidi likiwa ni la kutoa matamshi makali kwa Katibu Mkuu wa TFF.
Alisema kupata nafasi ya kuwa mmoja kati ya viongozi wa wajumbe wa kamati hiyo kutasukuma maendeleo ya soka la Tanzania kutokana na kwamba wao ndio watu wenye uwezo wa kupanga matumizi ya nani apate kiasi gani na nani hapaswi kupata gawio kubwa.
Hata hivyo Lucas alisema ofisi za TFF zipo wazi wakati wote kwa siku za kazi na kama barua hiyo itawafikia wataipeleka kwa wahusika ili kuangalia uwezekano wa kuyafanyia kazi maombi yake.
Wakati huo huo, Lucas alisema bado wanaendelea kujivunia uteuzi wa rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jama Malinzi kwa kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni(FIFA).
Alisema hatua hiyo ni kubwa sana kwa soka la Tanzania na kuna haja kwa watanzania wote wakamuunga mkono Malinzi kutokana na uteuzi alioupata kutoka kwa watu wenye jicho kubwa la kuendesha soka la dunia nzima.

Follow Us:
https://www.facebook.com/msechuJRhttps://www.instagram.com/officialhumphreymsechu/https://twitter.com/msechuhumphreymsechuhumphrey@gmail.com




Comments