Translate

KUTOKA BUNGENI: Bil 13.9 kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu

Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi 
bilioni 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 
wa shule za msingi nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
 za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameyasema hayo 
leo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge 
Viti Maalum, Mhe. Juliana Daniel Shonza juu ya mpango
 wa kuboresha miundombinu ya elimu vijijini kama vile 
nyumba za walimu pamoja na kulipa malimbikizo ya 
madeni ya walimu.

“ Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi 
Bil. 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 
kwa shule za msingi na shilingi bilioni 11.14 zimetengwa
 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 661 kwa shule za sekondari
,” alifafanua Jafo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, Serikali kupitia Mpango wa 
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMESII) imekamilisha
 ujenzi wa nyumba 146 kati ya nyumba 183 ambazo kila
 nyumba wataishi walimu Sita (6 multi-unit houses).

Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa nyumba hizo umegharimu
 shilingi bilioni 21.9 ambapo nyumba 37 zinaendelea  
 kujengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.5 na zinategemea
 kukamilika tarehe 30 Aprili, 2017.

Kuhusu ulipaji wa madeni ya walimu, Jafo amesema kuwa
 Serikali imeendelea kulipa madeni kadri yanavyojitokeza 
na kuhakikiwa ambapo katika mwezi Oktoba, 2015 Serikali 
ililipa madeni ya shilingi bilioni 20.12 kwa walimu 44,700 
na shilingi bilioni 1.107 zililipwa mwezi February, 2016 kwa
walimu 3221.

Follow Us:
https://www.facebook.com/msechuJRhttps://www.instagram.com/officialhumphreymsechu/https://twitter.com/msechuhumphreymsechuhumphrey@gmail.com




Comments