Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa Samwel Sitta amefariki dunia Hospitali Ujerumani saa 7:50 muda wa Ujerumani.
Mh. Samwel Sitta alikuwa akisumbuliwa na tezi dume ambayo ilipelekea kuathiri viungo vingine na kusambaa katika mwili mzima ambapo madaktari walijitahidi kuhitibu lakini ikashindikana na kupelekea umauti huo kumfika saa 7:50 muda wa ujerumani na saa 10:00 alfajiri kwa muda wa hapa Tanzania.Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.
Follow me:





Comments
Post a Comment