Translate

Rais wa Sudan Kusini kuwasili leo Tanzania

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir (pichani) leo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mbele ya Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Rais John Magufuli jijini Dar es Salaam.

Kiir anatarajia kuwasilia leo saa tatu asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja ambayo ataitumia kwa ajili ya kusaini mkataba huo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Rais huyo wa Sudan Kusini, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga alisema tangazo la kukubaliwa kuwa mwanachama wa EAC lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais Magufuli katika kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo uliofanyika Arusha mwezi uliopita.
“Kama mnakumbuka nchi ya Sudan Kusini ilikubaliwa kuwa mwanachama wa EAC, kwa hiyo ziara hii ya kikazi ni ya kusaini mkataba wa kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Kasiga.
Alisema baada ya kuwasili Rais Kiir atapelekwa moja kwa moja Ikulu kwa ajili ya kukutana na mwenyeji wake Rais Magufuli. Kasiga alisema Sudan Kusini ina fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinaweza kuzifaidisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo ikiwemo Tanzania endapo mipango madhubuti itawekwa kuzichangamkia.
“Fursa hizo ni pamoja na za kibiashara kwa sababu kila bidhaa inayotumiwa Sudan Kusini inaagizwa kutoka nje. Sudan Kusini inakabiliwa na uhaba wa chakula, huduma za kibenki na wataalamu mbalimbali,” alieleza. Kutokana na sababu hizo, aliwataka Watanzania kuhakikisha wanachangamkia fursa zinazopatikana katika nchi hiyo.
Katika hatua nyingine, Kasiga alisema serikali imewarudisha wajumbe na wafanyakazi wake waliokuwa katika balozi mbalimbali ambao mikataba yao imemalizika. Kasiga aliyabainisha hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari ambapo alisema, taratibu zinaendelea za kuhakikisha Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Burian ambaye amebaki anarudi.
“Mabalozi na wafanyakazi wote ambao mikataba yao imeisha wamesharudi nchini, isipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda. Bado sijapata taarifa za sasa hivi, lakini nafikiri anaweza kuwasili leo (jana),” alisema Kasiga.
Hivi karibuni, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilielezwa kuwa serikali inahitaji zaidi ya Sh bilioni 30 ili kuwarudisha watumishi ambao wako katika balozi mbalimbali ambao

Comments