Translate

Mbinu bora za ujasiliamali

Kwa kifupi,

Ujasiriamali ni uwezo wa kubaini na utayari wa kuanzisha shughuli ya kiuchumi bila kujali hatari za kibiashara zinazoweza kujitokeza. Pia katika uwezo huo wa kubaini,lazima uangalie fursa zinazokuzunguka pamoja na mazingira uliyonayo na aina ya shughuli ya kiuchumi unayotaka kuifanya au kuianzisha,kwa kufanya hivyo biashara yako utakayo ianzisha itafanikiwa.


Mbinu za kupata mitaji 

  1. Kuunda vikundi vya ushirika wa uzalishaji
  2.  Kuunda vikundi vya ushirika wa kuweka na kukopa
  3.  Kuwasiliana na wadau wa maendeleo (k.m. asasi za serikali na zisizo za kiserikali, taasisi za fedha, n.k.)
  4.  Kukusanya kidogo kidogo kutoka kwenye rasilimali binafsi.


Katika biashara yako ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo:-

  1. Kutoa huduma yenye kiwango na kudumisha kiwango husika
  2.  Kufahamu wateja wako na kuwaridhisha 
  3. Kufuata miongozo na kanuni za biashara husika
  4.  Kufahamu mazingira yanayozunguka shughuli zako
  5.  Kufahamu mahitaji ya bidhaa yako
  6.  Kufahamu nguvu ya kiuchumi ya wateja wako
  7. Uadilifu na uaminifu katika shughuli 
 Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara

Ni muhimu kuwa na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu mbalimbali, ili kumwezesha mjasiriamali kufuatilia gharama za uzalishaji na uendeshaji, kupata habari za masoko na wateja wa bidhaa zake.

  • Weka kumbukumbu ya kinachoingia na kutoka
  •  Weka kumbukumbu ya gharama za uzalishaji na uendeshaji 
  • Weka kumbukumbu na aina ya bidhaa na wateja wako.

Mwisho.
    Ni vyema kuwa unapitia kila siku ukawa unatathimini biashara yako ilikujua changamoto zilizopo  au ni maboresho gani unatakiwa uyafanye katika biashara yako ili kila siku iitwapo leo iwe kwenye ubora.

Comments