Translate

CONFIRMED: Huyu ndio kocha mpya wa Chelsea atakayejiunga na timu mwisho wa msimu 2015/2016

Chelsea imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio ConteChelsea imempa mkataba Conte ambaye atajiunga na timu hiyo baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika akiwa anaiongoza timu ya taifa ya Italia katika michuano hiyo. Kama utakuwa unakumbuka vizuri Antonio Conte aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2000, lakini amewahi kuvifundisha vilabu vya Juventus ya Italia kuanzia mwaka 2011-2014, Siena na timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Conte kwa sasa ana umri wa miaka 46.

Kwa sasa klabu hiyo ya chelsea ipo chini ya kocha wa muda Guus Hiddink, ambaye ataondoka  klabu hapo mwishoni mwa msimu huu

Comments