Translate

Bayern yakaribia kutawazwa mabingwa mara nne mfululizo

 
Bayern Munich yafungua mwanya wa pointi saba kileleni mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga, Borussia Dortmund nayo yatoshana nguvu na watani wao wa jadi Schalke 04 na kutoa mwanya kwa Bayern kutangaza ubingwa na mapema
Bayern Munich imesogea karibu na ubingwa wake wa nne mfululizo katika Bundesliga baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya VFB Stuttgart siku ya Jumamosi na kufungua mwanya wa pointi saba wakati ikibakia michezo mitano hadi mwisho wa ligi.

Borussia Dortmund inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, iliridhika na sare ya mabao 2-2 dhidi ya watani wa jadi Schalke 04 jana Jumapili wakati Hertha BSC Berlin , iliyoko katika nafasi ya tatu ilitoshana nguvu na Hannover iliyoko mkiani mwa ligi kwa mabao 2-2.


Nikitakiwa kuchagua kati ya ushindi wa mchezo wa watani wa jadi Derby na kufikia nusu fainali ya kombe la Uropa ligi , nitapenda kusonga mbele katika Europa League, amesema kocha wa BVB Thomas Tuchel katika mahojiano na kituo cha Sky kabla ya mchezo huo wa watani wa jadi.

Comments